.

.

.

.

Monday, August 31, 2009

ZITTO AJITOA

Mbunge wa kigoma Kaskazini na katibu mkuu wa chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Zitto Kabwe amejitoa kugombea uenyekiti wa chama hicho ili kulinda mshikamano na umoja ndani ya Chadema na kutekeleza busara za wazee wa chama hicho.
Habari zinasema Zitto Kabwe ameamua kuacha kugombea kutokana na vikao mbalimbali vya wazee wa chama hicho vilivyokaa na kumsihi asigombee ili kutokigawa chama hicho katika kipindi hiki ambacho uchaguzi mkuu unakaribia ili kutokigawa chama na kuendeleza mshikamano katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2010.
Zittio Kabwe hivi karibuni alitangaza kugombea uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, baada ya kutangaza nia yake hiyo kulitokea malumbano mengi katika vyombo mbalimbali vya habari kitu ambacho huenda kimepelekea wazee wa chama hicho kukaa na kumshauri Mb. Zitto kutogombea nafasi hiyo ili kulinda maslahi ya chama, mshikamano na umoja ndani ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment