.

.

.

.

Monday, September 07, 2009

LIYUMBA HAKUFIKA MAHAKAMANI

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, leo imeshindwa kuanza kusikiliza maelezo ya awali ya kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba baada ya mshtakiwa huyo kushindwa kufika mahakamani kutokana na kuugua.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali, Justus Mulokozi, umeiambia mahakama kuwa umepata taarifa kutoka kwa uongozi wa Magereza kwamba mshtakiwa ni mgonjwa na hivyo hataweza kufika kortini leo.
Amesema kutokana na kuugua huko, ameiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hadi Septemba 21 mwaka huu.
Kauli hiyo imeungwa mkono na upande wa utetezi na kulifanya jopo la mahakimu watatu kuahirisha kesi hiyo kama ombi la upande wa mashtaka lilivyotaka.
Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Edson Mkasimongo. Wengine ni Benedict Mwingwa na Lameck Mlacha.
Liyumba anakabiliwa na kesi ya utumiaji madaraka vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 200, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.

No comments:

Post a Comment