.

.

.

.

Thursday, October 22, 2009

MWANASHERIA MKUU MPYA ALONGA ...

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali aliyeapishwa jana, Jaji Fredrick Werema amesema hatafanya kazi hiyo kwa kushinikizwa na mtu au umma bali kulingana taaluma yake.
Jaji Werema aliapishwa jana katika viwanja vya Ikulu baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Johnson Mwanyika aliyestaafu kwa lazima.Wengine walioapishwa na Rais Kikwete ni Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju, Bw. David Jiro (Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini), Bw. Sazi Salula (Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na Bw. Mbarak Abdulwakil (Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).Mara baada ya kuapishwa kwake, Jaji Werema aliteta na waandishi wa habari na kuweka msimamo wake kuwa kufanya kazi kwa kufuata mtu au umma unavyosema ni kukiuka madili ya taaluma yake."Nitafanya kama nilivyoapa, wengi mmenisikia kwa hiyo kana nitafanya kinyume na nilivyoapa nitakuwa nimeingia katika maeneo mengine, hilo hata aliyeniteua (Rais Kikwete) analifahamu," alisema Jaji Werema.Jaji Werema ambaye anashika kiti hicho huku mtangulizi wake, Bw Mwanyika akituhumiwa kushindwa kuishauri serikali kuhusu mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond na kulingizia hasara taifa, alikataa kabisa kuzungumzia jambo hilo na kuwaomba waandishi waliotaka kujua jambo hilo kuliacha kwani bado liko katika machakato wa kupata ukweli. "Moja ya mambo nisiyoyapenda ni kuropoka na ni kosa kubwa kwa jaji kuropoka bila kufanya utafiti. Jaji akiropoka halafu jambo likaja kuwa siyo kuna madhara makubwa katika jamii, hivyo naomba niingie ofisini kwanza nione ofisi ilivyo ndiyo nizungumze hayo."Mikataba ni mambo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, na katika ofisi yangu kuna wanasheria wa kutosha hivyo naamini nitafanya kazi zangu vizuri kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 59 inavyosema," alisema Jaji Werema. Akizungumzia ufisadi, Jaji Werema alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kuwa kuwa tayari liko katika mkono ya sheria na halijatolewa maamuzi, hivyo si vema kulizungumzia kwa sasa."Unapomtaja mtu kuwa fisadi lazima uwe na ushahidi wa kutosha jamani nawaombeni msihukumu kabla hamjahukumiwa, hili zingatieni," alisema Jaji Werema.Aliwasa waandishi kutoandika habari ambazo ziko mahakamani na bado hazijatolewa maamuzi kwani kwa kufanya hivyo kuingilia uhuru wa mahakama na zinatoa hisia tofauti kwa umma na kuonekana maamuzi yatakayotolewa na mahakama kuwa si sahihi, bali yaliyoandikwa na kusemwa katika vyombo vya habari ndiyo sahihi.Jaji Werema alizaliwa April 10, 1954 na kusoma katika vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Uingereza, Marekani, Italia ambako alisoma mambo ya mikataba na Bolivia aliposomea mambo ya kuzalisha, kuuza na kusambaza umeme.

No comments:

Post a Comment