.

.

.

.

Monday, November 30, 2009

MAFUA YA NGURUWE MKOANI MWANZA

SERIKALI mkoani Mwanza imezifunga shule za msingi 150 na sekondari 27 wilayani Kwimba ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa mafua ya nguruwe ambao mpaka sasa umeathiri watu 221 wilayani humo.
Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya wilaya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbasi Kandoro aliyetembelea shule ya msingi Ilula jana, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ryoba Christopher Kangoye alisema uamuzi huo umechukuliwa ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo wilayani humo.
Alisema uamuzi wa kufunga shule hizo umeenda sambamba na kupiga marufuku minada na mgulio yote wilayani humo.
Tumeamua kufunga shule hizo kabla ya muda wake kwa sababu wanafunzi wanatoka nyumbani na kuja shuleni kila siku. Hali hii inaweza kuchangia kuongeza kasi ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mafua ya Nguruwe, alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Alisema agizo la kufunga shule hizo ambazo haliwagusi wanafunzi wa kidato cha kwanza na kidatu cha sita ambao alisema kutokana na umuhimu wao, wataendelea na masomo mpaka watakapofunga shule mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment