.

.

.

.

Friday, November 13, 2009

MAMA KIKWETE KWENYE SHOO YA UTEPE MWEUPE



Mke wa Rais mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na Maendeleo (WAMA) akimweleza jambo Balozi wa kimataifa wa Utepe na msanii na mwanamitindo wakati wa onyesho la mavazi lililoandaliwa na Taassi ya Utepe Mweupe.
Na Anna Nkinda – MAELEZOJumla ya dola za kimarekani 10,000/= zimepatikana kutokana na mnada wa nguo ya kike iliyotolewa na msanii na mwanamitindo wa Kimataifa Naomi Campbell katika maonesho ya mavazi ya Relief Tanzania yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Movenpick jijjini Dar es Salaam.Maonesho hayo yaliandaliwa na Naomi Campbell ambaye ni Balozi wa Kimataifa wa Utepe Mweupe kwa kushirikiana na Mustafa Hassanali ambaye ni mwanamitindo wa hapa nchini kwa lengo la kukusanya fedha ili kutunisha mfuko wa Mtandao wa Utepe Mweupe (The White Ribbon Alliance).Akiongea mara baada ya maonesho hayo Campbell alisema lengo la kufanya maonyesho hayo ni kupata fedha ambazo zitatumika katika kampeni ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.Kuhusu wabunifu wa mavazi na wanamitindo wa hapa Tanzania alisema anaridhishwa na kazi zao na wanajitahidi kufanya kazi nzuri kwa ufasaha mkubwa na kwa kujituma.Aliendelea kusema kuwa anaipenda nchi ya Tanzania kwa sasabu inavivutio vingi kama vile mbuga za wanyama, visiwa vya Zanzibar, mito, milima, maziwa na Bahari ya Hindi huku akisisitiza kuwa si mara ya kwanza kuja Tanzania na ana wa kuendelelea kuja hapa nchini.Katika maonyesho hayo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Banda walihudhuria.Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon Alliance) wenye takribani nchi wanachama 143 duniani ambao jana uliadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake unafanya kazi kubwa yakuhakikisha kuwa nchi wanachama zinaondokana na vifo vya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

No comments:

Post a Comment