.

.

.

.

Wednesday, November 18, 2009

WANAUME KAMA MABINTI (VISERENGETI)

Kijana wa mjini, Mwilu Mwilola ‘Silvanus’ ambaye hivi karibuni alifumwa kitandani akiwa na Miss Mwanza 2006-07, Aunt Ezekiel kabla ya kutimuliwa na aliyekuwa mchumba wake, Sarah, anakuwa kipimo cha kwanza kwa sababu ‘ishu’ yake bado haijapoa.Silva, alifumwa akiwa na Aunt kitandani, wote wakiwa watupu kabla ya vurumai kuchukua nafasi, kwenye nyumba aliyokuwa anaishi, Kinondoni, jirani na Leaders Club, Dar es Salaam Alhamisi ya wiki iliyopita.Habari ya kufumaniwa iliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, toleo lake la Jumamosi iliyopita kabla ya Ijumaa Wikienda kuandika ‘ishu’ ya Silva kutimuliwa na kuanza maisha upya, baada ya kunyang’anywa kila kitu na Sarah.Kwa ujumla, habari zilizothibitishwa na Sarah, ndugu pamoja na marafiki wa karibu, zinaeleza kuwa Silva alikuwa akilelewa na mchumba wake huyo wa zilipendwa na kuhudumiwa kwa kila kitu kabla ya kuachwa kwa aibu hapa ‘juzi-kati’.

‘Brazameni’ wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel Mbwana ‘Chalz Baba’ naye yumo kwenye ‘listi’ baada ya hivi karibuni, mwanamke aliyekuwa akiishi naye, Mariam Ramadhan kumtimua kwa maelezo kuwa ni msaliti wa penzi lao.Mariam, alimtimua Chalz baada ya brazameni huyo kuangukia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu ‘The History’.Awali, Mariam alikuwa anaishi na Chalz Masaki, Dar es Salaam lakini baada ya kumtimua, hivi sasa mwana-Twanga huyo ‘anaminya’ kwenye ‘geto’ lake, Kinondoni Block 41, Dar.

Mwanamuziki mwingine wa Twanga, Kalala Hamza Junior hasahauliki kwenye orodha, yeye akitajwa kuishi ‘kisupastaa’ mjini kutokana na fedha za mrembo wake, Mary.Mbali na fedha, kwa sasa Kalala Jr hajui taksi wala daladala, badala yake ‘anaosha’ jina mjini kwa gari la Mary aina ya Toyota Nadia.

Twanga inaendelea kubeba ‘listi’ ya wanaume wanaopenda kulelewa kwa kumnyooshea kidole mwanamuzi ‘The Powerful Vocalist’, Saleh Kupaza ambaye kwa muda mrefu aliishi kwa nguvu ya mke wake, Mama Ife kabla ya kutengana.Saleh na Mama Ife, walitengana mapema mwaka huu baada ya mwanamuziki huyo kufumaniwa akiwa na mwanamke mwingine gesti.Mama Ife, ndiye aliyetinga kwenye ofisi za gazeti hili na kueleza kuwa yeye na Saleh basi, kabla ya kutangaza ndoa na aliyekuwa Meneja wa Televisheni ya C2C, Bahati Singh.Baada ya kuachana, Saleh alitunga wimbo unaopatikana kwenye albamu ya Mwana Dar es Salaam, unaoitwa Sitaki Kupenda ikiwa ni stori ya kweli, akielezea machungu aliyoyapata baada ya kupewa kisogo na Mama Ife.

Mwimbaji na rapa ‘The Amazing Vocalist’, Msafiri Said ‘Diouf’ ni mwanamuziki mwingine wa Twanga ambaye anadaiwa kuwa na hulka za kulelewa, akihusishwa na kimwana anayeitwa Mary, ingawa penzi lao haieleweki liliishia njia gani.

Dogo anayefanya kazi na Bendi ya FM Academia hivi sasa, Hassan Shaban ‘TX Moshi Jr.’ yupo kwenye namba ya wanaume wa hulka hiyo, yeye akidaiwa kuwekwa kinyumba na muigizaji Shumileta.Inaelezwa kwamba hivi sasa TX Jr. hataki tena kuishi kwenye nyumba yao ya Keko, badala yake ameamua ‘kuminya’ na Shumileta, Tabata, huku akitanua mjini na gari la muigizaji huyo.

Risasi Mchanganyiko linazo ‘data’ kuwa muigizaji ‘Mwili Jumba’, Gladys Chiduo ‘Zipompa’ aliwahi kumuweka kinyumba mwanamuziki wa zamani wa Bendi ya Diamond Sound, Zola Ndonga ambaye aliondoka kama alivyoingia pindi walipotibuana.

Kizito wa Kundi la Wateule, Jaffari Ally Mshamu ‘Jaffarai’ anaingia mzima mzima kwenye namba ya wanaume wanaolelewa kutokana na uhusiano wake wa kimapenzi na Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Shyrose Bhanji.Kwa ujumla, penzi la Shyrose na Jaffarai siyo stori kutokana na kuandikwa mno na vyombo vya habari na inadaiwa kuwa nidhamu ya mwana-Hip Hop huyo ndiyo inayosaidia uhusiano wao kudumu mpaka leo.Katika uhusiano wao, Jaffarai amekuwa akipata huduma zote muhimu kutoka kwa Shyrose ambaye kutokana na kukolea kwa kijana huyo, huwa haoni ubahili ‘kukata pochi’ kumuwezesha ‘handsome boy’ wake.

Rais wa Bendi ya Akudo Impact, Christian Bella ‘Obama’ naye anatajwa kuwepo, akielezewa kwamba hivi sasa anapata matunzo yote kutoka kwa mwanamke anayefahamika kwa jina moja la Lillian.

Rapa wa FM Academia, Kitokololo a.k.a Kuku, pia anaongeza idadi ya wanaume wenye majina mjini ambao wanaishi kwa kulelewa na mademu zao, yeye akiwa amewekwa kinyumba na mwanamke aliyemzidi umri ‘jimama’, Sinza White Inn, Dar.Kabla ya kuhamia kwa mwanamke huyo, Kitokololo alikuwa anaishi na jimama lingine, Kinondoni, Dar kabla ya kutimuliwa kutokana na tabia yake ya ulevi wa kupitiliza kugeuka kero kwa mpenzi wake huyo.Risasi Mchanganyiko, hivi karibuni liliongea na Kitokololo ambaye alikiri kuhamia kwa jimama huyo, White Inn lakini akajigamba kwamba akiwa hapo, ni yeye ndiye ‘hukata pochi’ kwa ajili ya matumizi.

Mtangazaji wa Kituo cha Channel 10, Benny Kinyaiya anaingia moja kwa moja kwenye ‘listi’ kutokana na ile ‘ishu’ yake ya kutimuliwa na jimama na kutupiwa vyombo, ambayo iliandikwa magazetini.Katika sakata hilo, ilidaiwa kwamba Benny alikuwa akiishi kwa jimama hilo ambalo liliamua kumhudumia kwa kila kitu, lakini baadaye mwanamke huyo alimtimua kama vile hamjui baada ya penzi kutumbukia nyongo.

SOURCE : GPL

No comments:

Post a Comment