.

.

.

.

Wednesday, January 06, 2010

BEI YA PETROLI YASHUKA

MAMLAKA ya Udhibiti na Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta kuanzia leo kutokana na kuimarika kwa shilingi ya Tanzania.Taarifa iliyotolewa na EWURA na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Hatruna Maseba imeelza kuwa bei ya mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko wakati mamlaka hiyo ikihamasisha ushindani katika soko la dunia.Imeelezwa kuwa sababu za kushuka kwa bei hiyo ni kutokana na kushuka kwa bei katika soko la dunia na kutoteteleka wka thamani ya shilingi ya nchini ikilinganishwa na dola ya Marekani.Kutokana na hali hiyo sasa bei ya mafuta ya petroli imeshuka kwa asilimia 3. 33, dizeli (500 ppm) imeshuka kwa asilimia 2.48 dizeli (500ppm) imeshuka asilimia 2.56 na mafuta ya Taa asilimia 3.44."Taarifa hizi hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta, " ilisema sehemu ya taarifa hiyo.Pia imeelezwa kuwa kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ili mradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo.Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa vituo vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta."Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja ili kushamiri ushindani, " imesema sehemu ya taarifa.Bei ya mafuta ya petoli Dar es Salaam bei elekezi ni sh 1, 426 wakati bei ya kikomo ni sh 1, 533 wakati bei ya mafuta ya taa elekezi ni sh 958 na bei ya kimomo ni sh 1, 030.Kibaha bei ya mafuta ya petoli elekezi ni sh 1, 431 na bei ya kikomo ni sh. 1, 538 na bei ya mafuta ya taa elekezi ni sh. 963 na bei ya kikomo ni sh 1, 035, Bagamoyo bei ya mafuta elekezi ya petroli ni sh. 1, 438 na bei ya kikomo ni sh. 1, 545.Mkoa wa Morogoro bei ya mafuta petroli elekezi ni sh. 1, 451 na bei ya kikomo ni sh. 1, 560 wakati bei ya mafuta ya taa elekezi ni sh. 983 na bei ya kikomo ni sh. 1, 057.Aidha wanunuzi wameshauri kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe aina ya mafuta yaliyonunuliwa ba bei kwa lita ili kudhibiti mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo ama kuuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

No comments:

Post a Comment