.

.

.

.

Tuesday, April 06, 2010

ARSENAL NA BARCELONA NANI ZAIDI ?

HUKU zikikabiliwa na majeruhi wengi katika vikosi vyao, Barcelona na Arsenal leo zinaamua timu ipi itakuwa ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zikiwa na akiba ya mabao 2-2 kibindoni baada ya sare ya wiki jana mjini London, timu hizo ambazo zina majeruhi wengi, zinaweza kuwachezesha makinda Theo Walcott kwa upande wa Arsenal na Bojan Krkic wa Barca katika mchezo ujao.

Arsenal itakuwa mgeni wa Barcelona ambayo imempoteza mshambuliaji aliyepachika mabao mawili Emirates, Zlatan Ibrahimovic aliyeumia juzi.

Kutokana na maumivu hayo na baadhi ya wachezaji kuwa nje kwa kadi , makocha Arsene Wenger na Pep Guardiola watalazimika kufanya marekebisho katika vikosi vyao.

Arsenal itawakosa nahodha Cesc Fabregas, aliyevunjika mfupa wa mguu kwenye mechi ya wiki jana huku Barca ikimkosa Ibrahimovic, raia wa Sweden aliyekuwa mwiba mkali mjini London.

Guardiola alimchezesha Bojan Jumamosi katika ushindi mnono nyumbani wa mabao 4-1 dhidi ya Athletic Bilbao baada ya Ibrahimovic kujitoa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Bojan, 19 alifunga bao katika mchezo huo.

"Amekuwa akifunga mara kwa mara akicheza kama mshambuliaji. Ninahisi kuwa na deni kwake kwani amekuwa msaada kwetu," alieleza Guardiola. "Lakini, bado ni mdogo, ana mengi ya kujifunza. Hatuwezi kusahau kitu hiki."

Akiwa na Thierry Henry ambaye hajamridhisha, Guardiola , Bojan anaweza kuanza leo.

Pia, Barca itawakosa mabeki wake, Carles Puyol (kadi nyekundu) Gerard Pique, (kadi tatu za njano). Badala yao, watacheza, Gabriel Milito na Yaya Toure.

Eric Abidal alicheza mechi yake ya kwanza baada ya wiki sita kutokana na kuwa majeruhi alipoanza Jumamosi.

Baada ya Arsenal, Barca itakwenda Santiago Bernabeu kuikabili Real Madrid, mchezo wa Ligi Kuu, La Liga kuwania ubingwa, kitu ambacho Guardiola anasema kuwa hicho ki kipaumbele chake.

"Jumanne (leo) ni mchezo muhimu zaidi kwetu mwaka huu, kuliko hata ule wa Bernabeu," aliongeza.

Wenger , kwa upande wake atalazimika kumuanzisha katika mchezo huo, Walcott, 21, kutokana na kasi aliyo nayo winga huyo wa England.

Tayari anawakosa Andrei Arshavin na Fabregas kwa upande wa ushambuliaji na Robin van Persie ambaye hayuko tayari kwa mechi baada ya kuwa nje ya dimba tangu Novemba mwaka jana. Hivyo, ni jukumu la kocha huyo kuamua Walcott aanze au la.

Kocha huyo anahitaji ushindi au sare ya 3-3 au zaidi ili kufuzu kwa nusu fainali kwa mara nyingine msimu huu na huenda ikatumia udhaifu wa ukuta wa Barcelona huku safu ya ushambuliaji ya Barca ikiwa tishio kwa Wenger.

Arsenal haina majeruhi zaidi kutokana na mechi ya Jumamosi iliyoshinda kwa tabu 1-0 dhid ya Wolverhampton Wanderers 1-0 Jumamosi na kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Vikosi vinaweza kupangwa:

Barcelona: Victor Valdes, Daniel Alves, Gabriel Milito,Yaya Toure, Eric Abidal, Xavi, Seydou Keita, Sergio Busquets,Lionel Messi, Bojan Krkic, Pedro

Arsenal: Manuel Almunia, Bacary Sagna,Thomas Vermaelen, Sol Campbell, Gael Clichy,Tomas Rosicky,Alex Song, Abou Diaby, Samir Nasri, Theo Walcott, Nicklas Bendtner.

1 comment: