.

.

.

.

Tuesday, April 13, 2010

VIFO MKOANI KAGERA

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Kagera, akiwemo mama mmoja aliyejinyonga baada ya mume wake kuoa mke mwingine.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Henry Salewi alisema tukio la kwanza lilitokea kitongoji cha Busimba, katika Kijiji cha Nyakatanga Kata ya Rushwa wilayani Muleba na Georgia Joston (20) alifariki dunia kwa kujinyonga kwa shuka baada ya mumewe kuona mke mwingine.

Kamanda Salewi alisema maiti ya mama huyo iligunduliwa na majirani zake baada ya kukutwa akininig'inia juu ya mwembe ulioko katika shamba lake, Aprili 8 mwaka huu saa 6:00 mchana.

Alimtaja mme wa mama huyo kuwa ni Joston Lwakamgungu na kwamba chanzo cha kifo hicho ni wivu wa kimapenzi.

Katika tukio lingine, Mwalimu wa shule ya msingi Kibeta katika Manispaa ya Bukoba, Alchard Lukaka amekutwa amefariki dunia katika shamba lake lililoko eneo la Kashura.

Alisema taarifa za awali kutoka kwa mke wa marehemu Flora Alchard, zimeeleza kuwa marehemu alitoweka nyumbani Februari 28, mwaka huu na kuelekea kusikojulikana baada ya kuwa na ugomvi na mke wake.

Alisema mwili wa marehemu uligunduliwa Aprili 7, mwaka huu na Ofisa afya wa Mkoa wa Kagera, Helman Kabiligi ambaye alikuwa rafiki wa marehemu.

Alisema walipofika katika shamba hilo, waliona mwili wa mtu akiwa amelala chali na walipousogelea waligundua amefariki dunia na mwili huo, ukiwa umeoza.

Alisema mke wa marehemu alimtambua kuwa ni mumewe kutokana na nguo alizokuwa amevaa na kutoa taarifa polisi.

Tukio la tatu, mwendesha pikipiki, Hafidhu Kalori, mkazi wa Migera katika Manispaa ya Bukoba amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa gari.

Kamanda Salewi alisema ajali hiyo, ilitokea Aprili 11, mwaka huu saa 11:00 jioni katika barabara ya Kashozi Kata Nshambya katika manispaa hiyo.

No comments:

Post a Comment