.

.

.

.

Tuesday, June 22, 2010

MIAKA KUMI YA TWANGA PEPETA


Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mgahawa wa Hadees wakati alipozungumzia maadalizi ya sherehe za miaka kumi ya bendi yake ya African Stars inayotarajiwa kufanyika Juni 27 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa msanii wa n ngoma za asili kutoka Kenya anayeitwa Tonni Nyandudo.
Asha amesema kutafanyika maadamano yatakayowahusisha wanamuziki wa bendi hiyo pamoja na marafiki wa bendi hiyo maadamano yatakayoanzia katika ofisi za ASET na kuishia katika viwanja vya Leaders na kufuatiwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu, kukimbiza kuku, kuruka kamba , kuvuta kamba na kukimbia na magunia.
Baada ya michezo hiyo kutafuatia na onyesho kubwa litakalofanywa na bendi ya Africa Stars itakayopiga nyimbo zake kumi zilizobeba Albam zake hizo kumi huku wanamuziki kadhaa walioanzisha bendi ama kuwahi kufanya kazi katika bendi hiyo hiyo wakishiriki katika onesho hilo.
Amezitaja nyimbo zitakazopigwa na Albam zake kuanzi albam ya kwanza kuwa ni Kisa cha Mpemba, Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari 2005 Passworld, Mtaa wa kwanza na Mwana Dar es salaam huku kiingilio katika onesho hilo kikiwa ni shilingi 5000 kwa wote.

Wanamuziki waliokuwa wanzilishi wa bendi ya African Stars walikuwa ni Abuu Semuhando, Jesca Charles, Lwiza Mbutu, Bob Gad, Amigolas, Yahya Mkango, Jose Watuguru, Rogat Hega, Victor Mkambi, Adorf Mbinga na Banza Stone ambao wamethibitisha kushiriki katika onesho hilo.

No comments:

Post a Comment