.

.

.

.

Monday, June 14, 2010

MKE WA RAISI AKUMBWA NA KASHFA YA NGONO


Mke wa pili wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli amekumbwa na kashfa nzito ya kutoka kimapenzi na mlinzi wake, Phinda Thomo mkazi wa Dobsonville, Soweto.
Habari hiyo ambayo imeshtua watu wengi wa Afrika Kusini na Bara la Afrika kwa jumla, imetangazwa katika baadhi ya magazeti na redio nchini humo na tayari Rais Zuma amekwishaangukiwa kimila ili kuua ‘soo’.

Baadhi ya magazeti nchini humo yaliyoripoti tukio hilo ni pamoja na Kizulu Ilanga Newspaper, Durban Newspaper, mtandao wa Yellowpages na vyombo vingine Afrika.
Habari hizo zinadai kuwa familia ya mke huyo wa pili wa Rais Zuma imelazimika kumlipa (Zuma) fidia ya mbuzi mmoja mweupe baada ya kugundulika kuwa mke huyo aliisaliti ndoa yake kwa kutembea na mlinzi wake.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa utata upo kwenye ujauzito alionao hivi sasa mke huyo wa Rais na imedaiwa pia kuwa mke huyo, aliwahi kufukuzwa toka nyumbani kwa Zuma siku chache kabla ya Sikukuu ya Krismasi mwaka jana baada ya kugundulika alimsaliti.
Aidha, inadaiwa na vyombo hivyo vya habari kuwa mlinzi Thomo alijiua baada ya siri kufichuka kuwa alitembea na mke wa rais.
Ntuli ambaye hivi sasa yuko pamoja na Zuma katika safari ya kiserikali nchini India, ana mimba ya mtoto anayetarajiwa kuwa wa 21 wa Zuma.

Hata hivyo, maswali mengi yamezuka kuhusiana na ukweli wa baba wa mtoto huyo aliye tumboni mwake.
Taarifa hiyo inayodaiwa kusambazwa na wanafamilia inasema kuwa, Ntuli mwenye umri wa miaka 35 aliamua kufanya hivyo baada ya kukasirishwa na hatua ya Zuma kutangaza kuoa mke wa tatu.
Taarifa zaidi zinasema kwamba, Ntuli alimtolea lugha chafu mke wa tatu wa Zuma, Tobeka Madiba na pia alitishia kutohudhuria harusi yake iliyofanyika Januari mwaka huu.
Hata hivyo, alibadilisha uamuzi wake na kuhudhuria harusi hiyo lakini alifukuzwa na kurudishwa kwao wakati wa sherehe za kitamaduni za harusi hiyo.

Habari zinadai, Ntuli alisindikizwa na wazee wa kijadi hadi kwenye nyumba ya familia yake ambapo alikabidhiwa kwa wazazi wake.
Ntuli aliambiwa kuwa kitendo cha kuisaliti ndoa yake, kimeikasirisha familia ya Zuma na mizimu ya mababu na ili kuweka mambo sawa, Aprili mwaka huu, familia ya Ntuli ilienda kwa Zuma na kumlipa fidia ya mbuzi mmoja mweupe ambaye alichinjwa siku hiyo hiyo.

CHANZO: GPL

1 comment:

  1. Duuu huyu mlinzi ni hatari yaani anakula fast laid ahhn! no first lady sio mchezo afu mambo yao poa sana yaani akilipwa mbuzi mzee mzima anauchuna ndo yamekwisha hivyo.

    ReplyDelete