Baada ya kwisha vita vya Kagera mwaka 1979, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliamua kumjengea Mwalimu Nyerere nyumba ya kuishi, ikiwa kama zawadi kwake kwa ushindi wa vita hivyo, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa wakati huo. Nyumba hiyo, ambayo ilijengwa Butiama ilijengwa na kitengo cha ujenzi cha JWTZ.
Nyumba iliyojengwa na JWTZ inavyoonekana kwa nje
Ujenzi wa nyumba hii ulipoanza, wanajeshi walikatwa mishahara yao kuchangia gharama za ujenzi. Hata hivyo baadaye Serikali ya awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi ilichukuwa jukumu la kuendeleza ujenzi ambao uliisha wakati wa Serikali ya awamu ya tatu ya Rais. Benjamin Mkapa, na kukabidhiwa kwa Mwalimu Nyerere mwaka 1999.
Aliishi kwenye nyumba hiii kwa siku 14 tu kabla ya kwenda kwenye matibabu Uingereza ambako alifariki tarehe 14 Oktoba, 1999
No comments:
Post a Comment