.

.

.

.

Sunday, September 05, 2010

RATIBA YA TWANGA SIKUKUU YA IDD











Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” inatarajiwa kufanya maonyesho maalum katika kusherehekea sikukuu ya EID EL FITRI inayotarajiwa kusherehekewa siku ya IJUMAA tarehe 10 mwezi wa huu au siku ya JUMAMOSI tarehe 11 mwezi wa huu mwaka huu wa 2010.

Siku ya IDDI MOSI Mchana kuanzia saa nane Twanga Pepeta inatarajiwa kuanza na onyesho rasmi kwa ajili ya watoto ukumbini MANGO Garden, ambapo Zawadi nyingi zitatolewa kwa watoto watakaohudhuria, Usiku Twanga pepeta inatarajiwa kuwepo hapo hapo ukumbini Mango Garden onyesho likiwa rasmi kwa watu wazima mara baada ya onyesho la watoto kumalizika.

IDD PILI usiku kuanzia saa tatu Twanga Pepeta pia inataraji kupatikana ukumbini hapohapo Mango Garden. Twanga Pepeta itafanya onyesho siku ya IDD TATU katika ukumbi wa T.C.C Chang’ombe

No comments:

Post a Comment