Assalaam a'laykum,
Salama Trust inafuraha kuwatangazia kuanzishwa kwa jumuiya ya Tawhiyd Muslims Organisation ambayo makao makuu yake yapo Northampton.
Nia na lengo la jumuiya ya Tawhiyd ni ile ile ya kufuata na kuendeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (S.W.) na kufuata yale aliyoamrishwa Mtume wetu Muhammad (S.A.W.) kwa kufuata Sunna na Sharia za Kiislam.
Jumuiya ya Tawhiyd imeanza kutoa huduma za Maziko kwa Waislam wa UK na hivi sasa kwa wale ambao wameshasikia faida (benefits) zinazopatikana katika kujiunga na Mfuko wa Maziko wa Tawhiyd, tayari wameshajiunga na mfuko huo katika mikoa miwili mpaka mitatu ya UK ikiwemo London; na Jumuiya ya Tawhiyd inataraji kuwa na matawi mbalimbali katika miji ya UK kwa kutoa huduma za Maziko na kuwa kama Jumuiya mama ya Mfuko wa Maziko UK.
Tawhiyd yenyewe, tayari imeshajizatiti katika kutekeleza suala zima la Maziko, lakini itaweza kufikia malengo yake kikamilifu kwa kushirikiana na Jumuiya mbalimbali za Kiislam ambazo zipo UK kwa kuwapa mafunzo kamili ya kukafini maiti kwa njia za Kiislam na mafunzo mengineyo muhimu kuhusu Maziko iwapo jumuiya hiyo itahitaji.
Kuna jumuiya ambazo tayari zinazo mfuko wa maziko na baadhi ya jumuiya hizo zipo katika meza ya mkutano na Jumuiya ya Tawhiyd katika makubaliano vipi wataweza kufanya kazi pamoja ili mfuko uwe mkubwa si kwasababu nyingine ila kwa ajili ya kupatikana faida (benefits) nyingi kwa kiwango kidogo kwa manufaa ya jamii nzima na hususan pale mmoja wetu anapofikiwa na msiba.
Kama upo UK katika kijiji au mji ambao hakuna Waislam wengi au hakuna jumuiya inayotoa huduma za Maziko, tunakuomba wasiliana na Tawhiyd ili wachache mliopo katika mji huo mpate kujiunga iwapo mtaridhia. Jumuiya ya Tawhiyd itatoa mafunzo ya kukafini maiti iwapo mafunzo hayo yatatakikana, na si lazima uwe ni Jumuiya. Ama ikiwa ni Jumuiya, wasiliana na jumuiya ya Tawhiyd ili mpate kujua undani wake na vipi mtaweza kuwa pamoja katika jambo hili la Mfuko wa Maziko UK.
Kwa kumalizia, na kwa nia njema kabisa, ningependa kutoa rai kwa wale ambao wapo nje ya UK na nje ya Tanzania, wachukue mfano kama huu kwa kuanzisha Mfuko Wa Maziko na kamati maalum ili tunapofikwa na msiba kuwe na wepesi wa kushughulikia mwili wa maiti baada ya kututangulia mbele ya haki.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jumuiya ya Tawhiyd na njia ya kujiunga,bonyeza hapa au piga simu
07735075803 Abdullah (UK),
au
07985517163 Saleh Ali (UK),
au
07886535282 Saleh Jaber (UK).
Kwa niaba ya Tawhiyd,
Saleh Jaber
Mdhamini Salama Trust
No comments:
Post a Comment