.

.

.

.

Tuesday, April 19, 2011

BABU KUWA LIKIZO IJUMAA KUU HADI PASAKA

MCHUNGAJI mstaafu wa kijiji cha Samunge, Ambilikile Mwaisapile atasitisha huduma Ijumaa Kuu na Pasaka kutokana na siku hizo kuwa ni muhimu ya kukumbuka mateso ya Bwana Yesu Kristo kwa waumini wa dini ya kikristo nchini.

Aidha, watu wanaotoka Kanda ya Ziwa kwenda kunywa kikombe kwa Mchungaji huyo wametakiwa kufuata utaratibu uliowekwa ili kuondokana na kero zinazowakumba watu hao na magonjwa ya milipuko na vifo kwani hali iliyoko hivi sasa inatisha kutokana na msongamano wa watu na foleni kufikia kilometa 25.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidore Shirima amethibitisha uamuzi huo wa Mchungaji.

Pia aliwasihi watu wa Kanda ya Ziwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa kila njia kutoa watu 500 lakini pamoja na hilo, haikusadia kwa watu wanaotoka Kanda hiyo kamatiiliyoundwa kushughulikia mambo ya foleni kwa Babu inaangalia njia yenye watu pungufu na
kuwaongeza watu wa Kanda hiyo hadi 1,000 pale inapobidi ili waende kunywa dawa.

"Tunajitahidi kupunguza msongamano kule kwa Mchungaji, lakini watu wa Kanda ya Ziwa hawaelewi, tunasisitiza kwenda kule na kukaa foleni si tija na mnakiuka utaratibu uliowekwa; fuateni utaratibu hatutaki watu wafe kule wala msipeleke wagonjwa mahututi kwani kule si Hospitali ya Rufaa, fuateni utaratibu mtahudumiwa".

No comments:

Post a Comment