.

.

.

.

Saturday, April 23, 2011

MCHAKATO WA MISS UNIVERSE 2011 WAZINDULIWA

Ofisa Biashara na Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Upendo Richard, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kuanza mchakato wa kumtafuta mrembo wa Miss universe mwaka huu. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa kitaifa wa Miss Universe Maria Sarungi (kushoto) ni Mrembo anayeshikilia taji la Miss Universe 2010, Hellen Dausen.

Ofisa Biashara na Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Upendo Richard (kushoto), Mkurugenzi wa Kitaifa wa Miss Universe, Maria Sarungi, (katikati) na Mrembo anayeshikilia taji la Miss Universe, Hellen Dausen, wakishikana mikono kuashilia uzinduzi rasmi wa shindano la Miss Universe linalotarajia kuanza hivi karibuni. Uzinduzi huo ulifanyika jijini jijini Dar es Salaam.(Picha na Sufiani Mafoto)

No comments:

Post a Comment