.

.

.

.

Monday, June 06, 2011

MH.MBOWE ALALA LUPANGO SIKU MBILI




Mheshimiwa Freeman Mbowe ameachiwa kwa dhamana asubuhi hii baada ya kufikishwa mahakamani Arusha akitokea Dar es salaam ambako alikamatwa na polisi na kuwekwa rumande kwa siku mbili kabla ya kusafirishwa saa tisa usiku kwa ndege ya jeshi chini ya ulinzi mkali.

Mh. Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA na mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni, aliwekwa rumande siku ya Jumamosi baada ya kujisalimisha mwenyewe kituo cha kati cha polisi jijini Dar, baada ya mahakama ya Arusha kutoa amri akamatwe kwa kukiuka masharti ya dhamana, ya kutofika mahakamani hapo kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili wiki iliyopita.

Mh. Mbowe anakabiliwa na mashtaka ya kufanya mkutano bila ya ruhusa, na fujo, baada ya maandamano yaliyofanywa mapema mwaka huu huko Arusha.

Mahakama hiyo awali iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Bw. Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini) na wengine Bi. Josephine Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba wakamatwe.Pamoja na washtakiwa na wadhamini wao kutofika mahakamani ikiwemo Mawakili wao, Method Kimomogolo na Bw. Albert Msando pia hawakuwepo mahakamani wakati hati hiyo inatolewa, lakini washitakiwa Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwakamatwe kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Nai Steven, Mathias Valerian, John Materu, Daniel Titus, Juma Samuel, Walter Mushi, Peter Marua na Erick Makona.Hakimu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo wala mdhamini wake, hivyo Ofisa Inchaji wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama ni si vinginevyo.

“Wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo wanapatikana na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu. Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa Inchaji amkamate na kufikishwa mahakamani,” Hakimu Magesa aliamuruHabari zinasema pamoja na kuwepo umati mkubwa wa watu mahakamani, ambako pia ulinzi ulikuwa umeimarishwa maradufu, hakujatokea vurugu ya aina yoyote hadi tunakwenda hewani hivi sasa na kwamba kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 25 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment