.

.

.

.

Wednesday, July 20, 2011

ALI CHOKI AMNYAKUA AISHA MADINDA


Katika kile ambacho hakikutegemewa na wengi, mnenguaji wa siku nyingi sana ambae alikuwa akiifanyia kazi Twanga Pepeta Aisha Mbegu maarufu kama Aisha madinda ameihama rasmi Bendi hiyo ya The African Stars Twanga Pepeta na kukimbilia Extra Bongo ambayo iko chini ya Mzee wa Farasi ally choki..
Akitambulishwa rasmi kama mwana Extra Bongo..
sababu kubwa aliyoitoa Aisha alisema ni kutokana na safu ya wacheza show wa Extra Bongo ambao wengi wao amewazoea na amefanya nao kazi siku nyingi sana hivyo kukutana nao tena huku kutamfanya awe comfortable zaidi na kazi yake..
Kabla ya Aisha kuhamia Extra Bongo akitokea Twanga, tayari Extra Bongo ilikuwa imekwishanyakua wanenguaji wengi kwa mpigo kutoka Twanga akiwemo kinara nyamwela, Super danger, otilia pamoja na wengineo hivyo huenda hao ndio aliomaanisha aisha madinda kwamba ndio watu aliowazoea!!


PICHA NA HABARI KWA HISANI YA ZAMARADI

1 comment:

  1. dah na nyie wanamuzik mmezid kuhama bend lkn kwa dada aisha hakuna kingine alichofuata zaid ya pesa alitakiwa atangulize pia utu mbele

    ReplyDelete