.

.

.

.

Tuesday, August 30, 2011

IDD MUBARAK KWENU NYOTE WADAU


WAISLAMU wa Uingereza, wanaungana na wenzao duniani kusherehekea Siku Kuu ya Idd el Fitri, baada ya kumaliza ya faradhi ya funga ambayo ni nguzo ya nne kati ya tano zinazosimamisha dini hiyo. Hatua hiyo inafikia baada ya Waislam nchini kuungana na wenzao duniani kufunga mwezi wa Ramadhani.

Wakati hayo yakifanyika sisi tuchukue nafasi hiyo kuwapongeza Waislamu wote kwa kumaliza salama faradhi hiyo na pia kuwatakia sikukuu njema.Wengi wenu mlijikita vilivyo katika kufunga kwa bidii na kwa kuzingatia matakwa ya faradhi hiyo, ambayo malipo yake anayajua Mwenyezi Mungu pekee yake.

Matakwa ya msingi katika faradhi hiyo ni kumcha Mwenyezi Mungu kwa kufuata mambo mema aliyoyaamrisha na kuacha maovu aliyoyakataza si tu ndani ya kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, lakini pia hata baada ya mwezi huo wa toba.Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa katika kipindi chote cha Ramadhani, waumini wa madhehebu ya Kiislamu walionyesha umoja na mshikamano wao katika kumcha Mwenyezi Mungu kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujazana misikitini kwa lengo la kumwomba Mwenyezi Mungu kwa njia mbalimbali. Njia hizo ni pamoja na kusoma Qur’an na ibada nyingine.

Pia walishiriki katika kusikiliza mawaidha kuhusu mambo mbalimbali muhimu ya namna muumini wa Kiislamu anavyopaswa kuishi wakati na baada ya ibada hiyo.



Jambo nalotaka kulisema katika safu hii ni kuwasihi waumini wa Kiislamu waendelee kuyazingatia mafundisho ya Mtume Muhammad (SWA) kwa maana ya kuendelea kufanya mambo mema hata baada ya Mwezi Mtukufu.

No comments:

Post a Comment