.

.

.

.

Saturday, September 10, 2011

MELI YAZAMA ZANZIBAR NA KUPOTEZA MAISHA YA WENGI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho kikwete,akifuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,walifika katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar kuona maiti mbali mbali zilizofariki katika tukio la ajali Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini ikielekea Pemba.Picha na Ramadhan Othman IKulu.


Mv Spice. Photo by AFP
Waziri wa Mambo ya Ndani Nahodha akiangalia uokoaji.
Waokoaji wakiwa na baadhi ya miili iliyoopolewa, mpaka muda wa mchana miili 50 ilikuwa imeopolewa.
Wakazi wa Mji wa Zanzibar wakifuatilia uokoaji. Picha kwa hisani ya Vituko Zenji blogMeli ya Mv Spice iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja imezama usiku wa leo maeneo ya Nungwi ikiwa na abiria wanaokadiriwa kufikia zaidi 1000, wengi wao wanaofiwa kufa maji.


Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, vinasema meli ilikuwa imepakia mizigo na nabiria kuliko uwezo wake.MWENYEZI MUNGU AZIPUMZISHE ROHO ZA MAREHEMU WOTE MAHALA PEMA PEPONI

No comments:

Post a Comment