.

.

.

.

Wednesday, September 07, 2011

TUMSAIDIE HUYU NDUGU YETU

Constant Daud

Saumu Mwalimu
UGONJWA wa kansa unaomshambulia Mkazi wa Ubungo External, Constant Daud (39) kwa muda wa mwaka mmoja sasa amekuwa tishio kwa maisha yake kutokana na kutopata matibabu sahihi na sasa anaomba Wasamaria wamsaidie.

Akizungumza jana, Constant alisema ugonjwa huo ulianza kwa kukaza miguu.


“Ilianza kama utani mwaka jana mwishoni, nilikuwa napata maumivu ya mguu, nikawa natumia dawa tu za kupunguza maumivu hasa za kuchua huku nikiendelea na biashara zangu ndogondogo”, alisema Constant ambaye alikuwa ana kibanda chake cha kuuza chipsi.

Kwa sasa Constant amekuwa ni mtu wa kukaa ndani na muda wote akilala kitandani kutokana na maumivu makali anayoyapata.

“Siwezi tena kutoka nje, siwezi hata kwenda bafuni, nimekua ni mtu wa kusaidiwa kila kitu humuhumu chumbani, hali ya maisha imekuwa ngumu hata kula yetu imebadilika na kuwa ya shida.

“Msaada wetu unategemea watu wachache wanaokuja kutuona huku idadi ikipungua kila siku pamoja na Kanisa la KKKT Ubungo ambao kupitia Jumuiya ya mtaani wamekuwa wakitusaidia na pesa kidogo ya kununua chakula”, anasema kwa sauti ya chini huku akiugulia maumivu.

Alisema kutokana na hali mbaya ya ugonjwa wake, ameshauriwa kupata matibabu ya mionzi katika Hospitali ya Ocean Road lakini kutokana na kukosa kipato, inambidi alale akisubiri mwenye moyo wa kujitolea kumsaidia kupata matibabu.

“Nilienda nikapewa ushauri na kuambiwa natakiwa kuchomwa mionzi 30 pamoja na dripu ambazo zinauzwa Sh100,000 kwa dripu moja, sina fedha kupata matibabu hayo, madaktari waliniambia nahitaji kiasi kuanzia Sh2 milioni za matibabu, familia yangu ambayo ipo Mbeya ni maskini haiwezi kunisaidia zaidi ya kunipigia simu na kuniuliza naendeleaje”, aliongeza.

Constant anawaomba wasamaria wema kumsaidia kupata fedha ya matibabu pamoja na chakula.
Kwa yeyote anayeweza kutoa msaada wake awasiliane moja kwa moja na Constant ambaye anaishi Ubungo External kwa namba ya simu 0769- 367381. Ama kumtembelea nyumbani kwake hata kwa misaada ya chakula

No comments:

Post a Comment