.

.

.

.

Wednesday, October 19, 2011

RAHMA SWAI HATUNAYE TENA

MAREHEMU RAHMA SWAI RIP

Marehemu Rahma Swai (wa kwanza kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wenzake wa shindano la Miss Kanda ya Mashariki lililofanyika mjini Morogoro.

Rahma alifariki Okotoba 18,2011 mjini Mtwara baadaya kuugua ghafla na kupelekwa Hospitali na kufariki wakati akienbdelea na matibabu.

Mwili wa marehemu uliwasili jana nyumbani kwao Changanyikeni jijini Dar es Salaam na anataraji kuzikwa kesho mara baadaya kuwasili kwa mama yake aliyekuwa safarini Nchini Malawi kikazi na anatari kuwasili hii leo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Muandaaji wa Shindano la Miss Mtwara 2011, Rajab Mchata amesema Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania na baadhi ya warembo wa Kanda ya Mashariki na wale wa Miss Tanzania walifika kuomboleza msiba huo.

Hadi mauti yanamfika Marehemu Rahma (21) alikuwa ni mfanyakazi wa kituo cha Redio cha SAFARI RADIO FM cha mjini Mtwara.

KWA HISANI YA FATHER KIDEVU

No comments:

Post a Comment