



Mchezaji wa Yanga Davis Mwape leo amefanikiwa kuwafurahisha mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuifungia timu yake goli 1-0 dhidi ya Simba mahasimu wao wakubwa katika kipindi cha pili cha mchezo wa timu hizo Goli hilo pekee lililowafanya mashabiki wa Yanga kulipuka kwa vifijo na nderemo pamoja na kwamba walikuwa ni wachache kuliko wale wa Simba, wakati wakishagilia goli lao huku wakiwaacha wenzao wa Klabu ya Simba wakiwa wameinamia vichwa chini bila kujua la kufanya. Goli hilo pekee la Yanga limewafanya mashabiki wa Simba kuondoka uwanjani huku mpira ukiwa bado haujaisha jambo linaloonyesha jinsi walivyumizwa na goli hilo, wachezaji wa Simba wamekosa magoli mengi na walikuwa na uwezo wa kushinda mchezo huo lakini kitendo cha wachezaji wa timu hiyo kutokuwa makini golini kimewagharimu vya kutosha
No comments:
Post a Comment