.

.

.

.

Friday, October 28, 2011

ZITTO ANAENDELEA NA MATIBABU MIN ICU MUHIMBILI


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amebainika kuwa na vijidudu 150 vya malaria ambavyo vimemfanya alazwe Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), katika Hospitali ya Taifa(MNH)..

Wakati Zitto akilazwa ICU ndogo (Min ICU), mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Claradiana Mwatuka, naye amelazwa katika kitengo hicho akisumbuliwa na vidonda vya tumbo.Jana uchunguzi kuhusu Zitto ulibaini kuwa anasumbuliwa na malaria kutokana na kuwa na wadudu hao ambao ni wengi kwa mtu kuweza kuwahimili.Hata hivyo, akizungumza jana wodini kuhusu hali yake, Zitto alisema kwa kifupi tu, "naendelea vizuri, najisikia vizuri".

Awali, taarifa kutoka hospitalini hapo zilisema Katibu Mkuu Wizara ya Afya alipiga marufuku Zitto kusumbuliwa na kuagiza wote ambao walikuwa wakienda wasimsemeshe kwa muda mrefu wa dakika 20.

Kwa upande wake, Msemaji wa hospitali ya Muhimbili, Jezza Waziri, alisema Zitto baada ya kufanyiwa vipimo tangu alipofika hospitalini hapo amebainika kuwa na vijidudu hivyo 150.Hata hivyo, alisema uchunguzi zaidi kuhusu afya ya Zitto unaendelea na kuongeza kwamba majibu ya vipimo zaidi yataonyesha kama kuna matatizo mengine au la.

Alifafanua kuwa hadi sasa madaktari wamebaini tatizo kubwa linalomsumbua mbunge huyo ni malaria na kuongeza kwamba jitihada na taratibu zaidi za matibabu zimekuwa zikiendelea.


No comments:

Post a Comment