.

.

.

.

Friday, December 09, 2011

TUNAWATAKIA HERI YA MIAKA 50 YA UHURU WATANZANIA DUNIANI KOTE


WATANZANIA leo wanasherehekea miaka 50 ya Uhuru huku wakisifia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho na kutaja changamoto kadhaa zinazopaswa kufanyiwa kazi.Sherehe hizo ni kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika uliopatikana kwa njia ya amani Desemba 9, mwaka 1961 kutoka nchi ya Uingereza.Wakizungumzia maadhimisho hayo ya taifa kufikisha nusu karne kwa nyakati tofauti jana, watu hao wa kada tofauti walisema ingawa nchi imepitia misukosuko mingi, imefanikiwa mambo mengi, ikiwamo kuhakikisha tunu ya uhuru inalindwa.Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza kupata uhuru katika Ukanda wa Afrika Mashariki na ilikuwa Jamhuri mwaka 1962 kisha Aprili 26,1964 ikaungana na Zanzibar na kuzaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment