.

.

.

.

Friday, January 27, 2012

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA CLOUDS MEDIA GROUPMwenyekiti ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Peramiho,Mh Jenista Mhagama akizungumza jambo mbele ya kamati hiyo (haipo pichani) pamoja na uongozi wa Clouds Media Group mapema jana,Mikocheni jijini Dar,ambapo kamati hiyo imefanya ziara ndani ya kampuni hiyo na kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo.Aidha Mh Mhagama ameisifu na kuipongeza kwa kiasi kikubwa kampuni hiyo kwa utendaji wao mzuri wa kazi na pia kaitoa nafasi kubwa ya ajira kwa vijana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga akitoa historia fupi ya kampuni hiyo ikiwemo sambamba na utendaji kazi wake na mengineyo mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii iliyofanya ziara ndani ya kumpuni hiyo na kujifunza/kujionea mambo mbalimbali ya kiutendaji.
Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Mh Jonh Komba akieleza kuwa yeye ndiye muanzilishi wa kipindi cha Leo Tena,tangu enzi za Marehemu Amina Chifupa (Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin),ambacho kinaendelea mpaka sasa,Mh Komba alikuwa akizungumza hayo ndani ya kipindi cha Leo Tena wakati kamati hiyo ilipotinga ndani ya studio hizo na kujionea mitambo mbalimbali ya kisasa inavyofanya kazi.Pichani shoto ni Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Dina Marios
Mh Jenista Mhagama akiwapongeza watangazaji wa kipindi cha Leo Tena,shoto ni Mtangazaji wa kipindi hicho Bi Gea Habib a.k.a Mama wa heka heka na kulia ni mtaraishaji wa baadhi ya vipindi vya Clouds Fm,Simalenga
Mh Jenista Mhagama akizungumza jambo ndani ya studio za clouds fm akiwa sambamba na kamati yake huku kipindi cha Leo Tena kikeendelea.
Mmoja wa mainjinia wa Clouds TV,Mebb Hadhad akifafanua jambo kuhusiana na urushaji wa matangazo ya TV mbele ya kamati hiyo ambayo haipo pichani.
Mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akielezea jambo mbele ya kamati ya bunge ya Maendeleo ya jamii kuhusiana na utendaji kazi wa kituo cha Clouds TV na mambo mbalimbali yahusuyo mfumo wa masafa ya digitali ambayo kituo hicho inatarajia kujiunga nayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Clouds TV akifafanua jambo kwa kamati ya Bunge ni namna gani wanaandaa vipindi vya TV
 
Mh Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Juhyna Ajmy Kusaga ambao ndio waandaaji bingwa wa matamasha mbalimbali hapa nchini,ambapo kamati ya bunge ya Maendeleo ya jamii pia ilizitembelea ofisi hizo zilizopo ndani ya jengo la Clouds Media Group.
Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kikiongozwa na Mwenyekiti wake Mh.Jenista Mhagama wakiendelea na majadiliano kuhusu mambo mbali mbali kuhusiana na kampuni ya Clouds Media Group sambamba na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga akiwatambulisha baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

No comments:

Post a Comment