.

.

.

.

Saturday, March 10, 2012

MAMBO YA MULTICHOICE BONGOMeneja Mkuu wa Multchoice Tanzania Bw. Peter Fuel
akifurahia jambo na Meneja wa Uendeshaji Ronald Shelukindo wakati wa hafla ya wateja iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake, katika siku hii ya leo ving'amuzi vya DSTV vinauzwa kwa silingi 120.000 pamoja na kukuunganishia nyumbani kwako na ofaa hii ni ya leo tu.
Hafla hiyo inafanyika katika ofisi za Multichoice zilizopo Saint Peter Oysterbay jijini Dar es salaam.Mwanafunzi Diana Kimaro wa Chuo Kikuu cha Nilai Malasia akisomea masuala ya biashara ambaye yuko katika benki ya NMB kwa mazoezi akimpatia huduma mmoja wa wateja wa benki ya NMB aliyefika katika hafla hiyo, Benki ya NMB pia imeshiriki katika hafla hiyo kwa ajili ya kuwaelezea wateja wao huduma mbalimbali wanazozitoa.
Watoto wakicheza
Wanenguaji wa kiume wa bendi ya African Stars wakicheza katika hafla hiyo.
Mwimbaji wa bendi hiyo Lwiza Mbutu akiimba pamoja na wanamuziki wenzake katika hafla hiyo.
Meneja uendeshaji wa Multchoice Ronald Shelukindo akizungumza na wateja wa kampuni hiyo katika hafla hiyo.
Wateja mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wapata burudani mbalimbali.
Baadhi ya wateja pia wameongozana na watoto wao katika kuonyesha upendo.
Kulia ni Ronald Shelukindo Meneja Uendeshaji, Barbara Kambogi Meneja Uhusiano na katikati ni Orest Kawau kutoka African Media Group.
Mdau Julio Batalia akitangaza bidhaa yake ya PayPoint katika hafla hiyo.
Wadau kutoka benki ya NMB nao wakiwa katika hafla hiyo tayari kwa kuelimisha wateja juu ya huduma zao.

picha zaidi tembelea http://www.fullshangweblog.com/

No comments:

Post a Comment