.

.

.

.

Thursday, May 03, 2012

RAIS ATEUA WABUNGE WAPYAJaneth Mbene


James Mbatia.

Wakati Baraza jipya la Mawaziri likizubiriwa kwa hamu, Rais Jakaya Kikwete amewateua Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Sospeter Muhongo na Mama msomi wa siku nyingi, Janeth Mbene kuwa wabunge. Ifuatayo ni taarifa rasmi ya Ikulu iliyotufikia hivi punde.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wabunge hao wapya ni Profesa Sospeter Muhongo, Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia.
Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam. 
3 Mei, 2012

No comments:

Post a Comment