.

.

.

.

Wednesday, October 31, 2012

KIINGILIO LAKI MOJA KUONA FAINALI ZA REDDS MISS TANZANIA 2012

FAINALI za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza jijini D’salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema maandalizi yote yamekamilika na kila kitu kipo tayari na leo tupo hapa kuwatangazia Watanzania na washika dau wote wa tasnia ya Urembo kuwa tiketi kwa ajili ya shindano letu la mwaka huu zipo tayari na zipo kwa idadi maalum na leo hii zinaanza kuuzwa katika vituo tulivyovipendekeza kulingana na maoni ya wadau Kutokana na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila tiketi itagharimu kiasi cha shilingi laki moja (100,000) za Kitanzania. Katika kufanikisha shindano hili kutakuwa na vitu tofauti na miaka ya nyuma na tutarajie kuona shindano lenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya warembo wetu ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini

Vituo vinavyoanza kuuza tiketi hii leo ni. Stears samora Regency Park Hotel, Rose Garden Mikocheni, Shear Illusion-Mlimani City, Giraffe Hotel, Ubungo Plaza na ofisi za Lino.

Nitoe rai kwa wapenzi wote waweze kupata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu kwa sababu ya kikomo cha tiketi kilichopo kama tulivyotangaza awali


 Kwa upande wa burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa na wasanii nguli hapa nchini kama:
 1) Diamond Platnumz 2) Winfrida Josephat’Rachel’ 3) Wanne star ngoma troupe

Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo yanayojulikana kama [Fast Tract] Tayari washiriki 5 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika kundi la Warembo 15 Bora. [Top 15 Finalist] Washiriki hao ni Lucy Stephano – Miss Photogenic Magdalena Roy – Top Model Mary Chizi – Top Sport Woman Babylove Kalalaa – Miss Talent City sports lounge-iliyopo posta mpya mkabala na mnara wa askari. Happiness Daniel – Miss Personality Mwisho napenda kutoa shukrani zangu kwa wadhamini wetu ambao ni TBL kupitia kinywaji chao cha Redds Original,Star Tv na Giraffe Hotel


 HASHIM LUNDENGA. MKURUGENZI

No comments:

Post a Comment