.

.

.

.

Friday, October 12, 2012

TAFRIJA YA PPF YAFANA



Baada ya kushiriki kwa siku mbili mfululizo kwenye mkutano huo, Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF ambaye pia ndio mratibu wa mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa mfuko huo, Lulu Mengele, (Katikati), akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake, kwenye tafrija hiyo iliyoandaliwa na NBC.
 
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mkoani Arusha, (Kulia), akipoz kwa picha na mwandishi habari wa Channel Ten mkoani humo, Jamila Omar, wakati wa cocktail party iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wajumbe wanaohudhuria mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wan PPF Alhamisi usiku Oktoba 11, 2012, kwenye hoteli ya Kibo Palace jijini humo. Mkutano bhuo wa siku tatu uliowaleta pamoja zaidi ya wajumbe 700 kutoka ndani na nje ya nchi, utakamilika Ijumaa Oktoba 12, 2012
Marubani wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kutoka kushoto kwenda kulia, Heladius Kiyango, Weston Kipangula, Charles Tawete, Thomas Salu, Frank Mapunda na John Methew, nao walikuwepo
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe Jumapili, Flora Wingia, (Kulia), Jane Mihanji, (Wapili kulia), wakiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, David Mattaka
Lulu (Kulia) na wafanyakazi wenzake wa PPF
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhan Dau, (Wapili kulia), akiwa na viongozi wa Jukwaa la Wahariri, Mwenyekiti, Absalom Kibanda, (Kulia), Katibu wake, Nivile Meena 
Wafanyakazi wa PPF na wageni wengine waalikwa wakiwa katika pozi
Mshereheshaji mashuhuri nchini, Mzee Mavunde, (Kushoto), akijiunga kwenye bpoicha na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, katika picha hii ya kumbukumbu

No comments:

Post a Comment