.

.

.

.

Monday, November 26, 2012

SHARO MILLIONEA HATUNAYE TENAMsanii/Muigizaji/Mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioti (27) maarufu SHARO MILIONEA amefariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe, amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema kuwa marehemuamefikwa na umauti baada ya gari lake aina ya Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.

Hili ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.
Kamanda Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku wa Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

Akisimulia zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa akiendesha gari hilo na alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali kumfika akiwa katika kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.

“Marehemu ndie alikuwa akiendesha gari lile, na lililopopinduika yeye alirushwa nje lkupitia kiooo cha mbele na umauti kumfika hapo hapo” alisema Kamanda Massawe.

Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.

Inakumbukwa kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya utembeaji na uongeaji alipata al;inusurika katika ajali nyinge mapema mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu akirejea Dar es Salaam.


MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI

1 comment:

 1. INALLILLAH WAINAILLAH RAAJIUNN
  ckuzote 2napaswa kujua kwamba maisha yana mwanzo na mwisho wake,na kifo hakichagui mtu,kabila,umaarufu,rangi,umackin wala utajri wako,ila hukuchukua pale wakati unapofika.
  sasa 2natakiwa 2jifunze kupitia hii misiba ya ndugu zetu.
  Na 2fanye ibada kwa wingi kwani muda wwte na cc ni wasafir
  CHUKUA HATUA,KIFO HAKINA HURUMA

  ReplyDelete