.

.

.

.

Friday, December 21, 2012

LULU KUENDELEA KUSOTA RUMANDE


 Lulu akisindikizwa na maaskari kuelekea mahakamani mapema leo
Baadhi ya watu waliofika mahakamani hapo kusikiliza case hiyo
---
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salam leo imefunga jalada la kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa Filamu nchini ELIZABETH MICHAEL maarufu kama LULU tayari kwa kulipeleka mahakama Kuu ya Tanzania ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.

Kabla ya kuanza kusomwa kwa maelezo ya kesi hiyo ambapo LULU hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO amemtaka wakili wa Serikali kutaja idadi ya mashahidi watakaotoa ushahidi wao wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

Wakisoma kwa awamu maelezo ya mashahidi wa kesi hiyo Mawakili wa Serikali katika kesi hiyo wamesema kuwa wanao mashahidi Tisa wanaotarajia kuwatumia kwenye kesi hiyo na kubainisha kuwa shahidi namba moja katika Kesi hiyo ni SETH BOSCO kijana aliyekuwa akiishi na marehemu STEVEN KANUMBA.

 Katika maelezo ya SETH yaliyosomwa mahakamani hapo imeelezwa kwamba siku ya tukio KANUMBA alimtaka asitoke ili watoke pamoja lakini ilipofika majira ya saa tano usiku alisikia vurugu chumbani kwa KANUMBA ambako alikuwa na mpenzi wake ELIZABETH MICHAEL na baada ya muda alibaini kulikuwa na ugomvi baina ya wawili hao huku mlango ukiwa umefungwa.

Maelezo hayo yamesema kuwa baada ya muda LULU alitoka chumbani kwa KANUMBA na kumtaarifu kuwa KANUMBA ameanguka ndipo aliingia chumbani na kumkuta akiwa ameegemea ukuta pembezoni mwa mlango huku povu likimtoka mdomoni na kuamua kumlaza chini kabla ya kuomba msaada.

Mashahidi wengine wanaotarajia kutoa ushahidi wao wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa ni SOPHIA KASSIM mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi KANUMBA, Madaktari watatu, maofisa wa polisi watatu, afisa uhamiaji ambaye ni shemeji wa KANUMBA na MORIS SEKWAO kijana aliyempakia LULU kwenye gari yake muda mfupi kabla ya kukamatwa.

Baada ya kusomwa kwa maelezo ya mashahidi wote wakili huyo wa Serikali amesoma maelezo ya LULU na kubainisha kuwa walianza uhusiano wa kimapenzi Januari mwaka huu ambapo walikuwa na kutokuelewana katika baadhi ya nyakati hasa pale mmoja anapompigia mwenzake simu na kutopokelewa kwa wakati.

 Baada ya maelezo yote kutolewa na kukamilika Hakimu wa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO amezishukuru pande zote na kumkata LULU atoe maelezo ya nyongeza kama anayo ambapo LULU alisema hana maelezo yoyote.

Hakimu MMBANDO amemtaka LULU kuendelea kubaki Lumande mpaka hapo tarehe ya kesi itakapotajwa na mahakama Kuu ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment