.

.

.

.

Tuesday, January 29, 2013

LULU MICHAEL AACHIWA KWA DHAMANA



Msanii wa movie Elizabeth "Lulu" Michael tayari amerudi uraiani  baada ya kuachiwa kwa dhamana leo hii katika mahakama kuu jijini Dar. Licha ya kukamilisha kwa masharti yote aliyopewa jana ikiwa ni pamoja na  kutoa milioni 20 kwa wadhamini wawili,  kuripoti kila mwanzo wa mwezi na kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo, Lulu hakufanikiwa kutoka jana hiyo hiyo kwa kile kilichoripotiwa kutokuwepo kwa msajili wakati huo, hivyo kumlazimu kurudi gerezani
Lulu (katikati)  akiwa mwenye majonzi na furaha hapa akitokwa na machozi wakati msemaji wa familia Msanii Dr Cheni akizungumza . Lulu amewaomba watanzania wote wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi yake bado inaendela.

 LULU na Mama yake mzazi ndani ya gari tayari kwa safari ya kurudi nyumbani
Wakili wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza kwasababu case bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe tarehe ya Lulu kurudi mahakamani.

No comments:

Post a Comment