.

.

.

.

Saturday, February 09, 2013

TAARIFA TOKA FASTJET


Kama majibu kwa ripoti za kupotosha za hivi karibuni katika vyombo vya habari, David Lenigas, Mwenyekiti wa kampuni ya fastjet na Mwenyekiti wa Five Forty Aviation Limited tawi la Kenya (“Fly540 Kenya”), anathibitisha kuwa hakuna makubaliano yoyote halisi yanayohusu Leseni ya Nembo, Makubaliano ya kifursa au yale ya kimenejimenti kati ya Fly540 Kenya na Fastjet au kampuni yoyote inayohusiana na Fly540 Afrika.
 Matamshi yaliyofanywa na Don Smith, Mkurugenzi wa Fly540 Kenya, kuashiria kuwa anayo haki ya kuondoa nembo na pia leseni ya uendeshaji hayafai na hayana msingi. Bodi ya wakurugenzi ya Fly 540 Kenya haijawahi kukutana kwa ajili hata ya kufikiria suala hili na hii imethibitishwa na wakurugenzi wengine. Imetambulika kwa mapana na umma wa Tanzania kuwa suala hili si kitu kingine bali jaribio la kuhujumu sifa na uaminikaji katika kibiashara.

 Fastjet ingetaka kuvishauri vyombo vya habari na abiria ambao husafiri nasi katika Afrika nzima katika ndege za fastjet, ndege za Fly540 au ndege za Fly540  Afrika, kuwa, tunatazamia kupanua shirika letu lenye gharama za chini ili liwepo katika bara zima la Afrika.

Hadi sasa, tunakaribia idadi ya maombi ya kusafiria ya abiria 100,000, ambapo 30% wamelipia shilingi za kitanzania 32,000 tu kwa ajili ya tiketi zao. Vile vile, tunafanya kazi kwa kuzingatia muda na hatujakuwa na safari zilizofutwa au zilizobadilishwa huku ndege zetu nyingi zikiwasili ziendako kabla ya muda uliopangwa.

No comments:

Post a Comment