.

.

.

.

Wednesday, March 13, 2013

ALBUM MPYA YA BEN POL IKO NJIANINa Elizabeth John

MKALI wa muziki wa RnB nchini Tanzania, Bernad Paul ‘Ben Pol’ anajipanga kuachia albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ben Pol Love CD’ ambayo itakua na jumla ya nyimbo 16.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ben Pol alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo, ambayo anaamini ataisambaza sokoni mwishoni mwamwezi huu.

Alisema kazi hiyo itakua na mchanganyiko wa nyimbo za zamani na mpya ambazo bado hazijaanza kusika katika vituo mbambali vya redio.

“Naomba mashabiki wa kazi zangu wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hiyo ambayo naamini itawaburudisha wapenzi wangu kutokana na kuwa na nyimbo nyingi ambazo zilifanya vizuri katika soko la muziki huu,” alisema Ben Pol.

Mbali na kazi hiyo, Ben Pol alisema yupo katika mchakato wa kutengeneza video ya wimbo wake wa ‘Pete’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na kwamba mwisho wa mwezi huu ataisambaza kazi hiyo.

Licha ya kutamba na kibao chake cha  ‘Pete’, Ben Pol alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Nikikupata, Number One Fun, Samboila na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo

No comments:

Post a Comment