.

.

.

.

Thursday, May 23, 2013

MISA YA SHUKURANI YA MAREHEMU WILLIAM MUGURUSI

                       MAREHEMU WILLIAM VEDASTUS MUGURUSI           (1943 – 2013) 

Familia ya Marehemu, Bwana William Vedastus Mugurusi
wa Kijitonyama Dar es Salaam, inapenda kutoa shukurani zake za dhati kwa wale
wote walioshiriki nao katika kumuuguza na hatimaye kifo cha mume, baba, kaka na
babu yao mpendwa kilichotokea siku ya Jumanne tarehe 16.04.2013 katika hospitali  ya AMI Wellness Center na kuzikwa Ijumaa
tarehe 19.04.2013 katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.


Shukurani za pekee ziwaendee madaktari wote na wauguzi
wa hospitali za Apollo,(India) Aga Khan na Ami Wellness Center ambao walijaribu
kwa kadri ya uwezo wao kuokoa maisha ya mpendwa wetu; Uongozi na timu nzima ya
Globe Accountancy Service (GAS) kwa ushirikianao wao wa hali na mali; Mapadri
na wahudumu wote wa Kanisa Katoliki kwa huduma za kiroho; AAR, FHI360, ndugu,
jamaa, marafiki, wanajumuiya ya Mt. Damiano Mfia Dini, na majirani wote.


Kutokana na ukweli kwamba siyo rahisi kumshukuru kilammoja kwa jina, tunapenda kuwahakikishia kwamba tunathamini ushiriki wa kila mmoja kwa njia ya pekee, ushiriki ambao umeendelea  kutupa faraja wakati wa kipindi hiki kigumu.
Tunawasihi tafadhali kila mmoja apokee shukrani zetu za dhati katika uzito ule
ule.
Kutakuwa na misa ya shukrani tarehe 25 May 2013, saa 4 asubuhi nyumbani kwa marehemu William Vedastus Mugurusi, Kijitonyama.  


WOTE MNAKARIBISHWA.

No comments:

Post a Comment