.

.

.

.

Monday, May 13, 2013

UZINDUZI WA MSIMU MPYA WA CLOUDS FM DODOMA WAFUNIKA


 


 Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri jioni ya leo wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.


 Msanii mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa mji wa Dodoma alipowaangushia maneno kadhaa na umati kulipukwa na mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao mpya.
 Maelfu ya Watu wakiwa ndani ya uwanja wa jamhuri wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.

Mkurugenzi wa vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri jioni ya leo,wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea,Nape alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha maelfu ya watu.
 Palikuwa hapatoshi uwanja wa jamhuri Dodoma .Picha na Habari kwa hisani ya SHAFFI DAUDA

No comments:

Post a Comment