.

.

.

.

Tuesday, July 09, 2013

KUELEKEA MFUNGO WA RAMADHANI ........

Katika kuelekea Mfungo Mtukufu wa Ramadhani, bei ya vyakula inaonekana kuwa ya kawaida huku wafanyabiasha katika baadhi masoko jijini Dar es Salaam wakisema hawatarajiI kama itapanda kwa kuwa kwa sasa ni msimu wa mavuno.
Mfanyabiashara katika Soko la Kariakoo, Sadiki Salehe alisema kuwa bidhaa za maboga zimeshuka sana kwa kipindi hiki kwa kuwa zamani boga moja liliuzwa Sh4,000 mpaka Sh6,000 lakini kwa sasa yanauzwa Sh2,000 mpaka Sh3,000 hivyo hatujui bei hii kama itapanda au la
Hata hivyo katika Soko la Kisutu pamoja na Buguruni bei za bidhaa zimekuwa zikilingana ,mkungu wa ndizi ni Sh2,0000, ndoo moja ya viazi Sh 3,500 mpaka Sh3,000, vile vile viazi vitamu vinauzwa Sh50,000 mpaka Sh 45,000 na bei ya rejareja inaazia 1,000 mpaka Sh2,000 kwa fungu.
Kwa upande wa magimbi na mihogo kwa kiroba ni Sh3,0000 na kwa bei za rejareja ni Sh1,000 hadi Sh 2,000” alisema Abdallah Bakari.
Wafanyabiashara hao walisema wana imani kasma hali itaendelea kama ilivyo Ramadhani itakuwa nzuri.

No comments:

Post a Comment