.

.

.

.

Wednesday, August 28, 2013

MWEKEZAJI KUFUNGA MASHINE ZA KISASA "JNIA "

Mwekezaji Sheikh Salim Abdullah ametangaza kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JNIA) kwa kufunga mashine za kisasa, ili kuimarisha usalama katika eneo hilo. Sheikh Abdullah ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Maendeleo na Uwekezaji ya Al-Harathy ya Oman, alitangaza hatua yake hiyo jana, baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huo, ambapo alisisitiza mashine zilizopo uwanjani hapo kwa sasa uwezo wake kiutendaji na kiusalama ni mdogo. “ Mashine hizi uwezo wake ni mdogo, dunia tunayoishi sasa imetawaliwa na magaidi uwanja wa ndege ni eneo muhimu ambalo linapaswa kulindwa kwa uhakika, mizigo inabidi kukaguliwa kwa umakini zaidi kwani wanaweza kuweka mabomu au vitu vingine vya hatari wakasababisha madhara makubwa alisema na kuongeza:
“Nimekuja kuwekeza hapa kwa kuitikia mwito wa Rais Jakaya Kikwete, amechoka sana inabidi sisi tumsaidie, ana nia nzuri ya kuhakikisha nchi hii inakuwa kiuchumi inabidi tumsaidie kuwekeza katika maeneo kama haya” alisema. Katika hatua nyingine mwekezaji huyo ametangaza kuwekeza ndege nane kwenye Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), mradi ambao unatarajiwa kugharimu dola za Marekani 100 milioni.
“ Tunanunua ndege nane ambapo nne ni aina ya Embraer ERJ-175 za Brazil na nyingine nne aina ya Mbombardier,kwa kuanzia tunapeleka vijana 10 wa kitanzania kwenda kusomea jinsi ya kuongoza ndege hizo” alisema.

No comments:

Post a Comment