.

.

.

.

Thursday, July 30, 2015

WAZIRI Mkuu Wa Zamani Mh. Edward Lowassa Kuomba Kuwania Urais Kupitia CHADEMA WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, (kulia), akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba kuwania urais kupitia CHADEMA, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe, kwenye makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2015. Mh Lowassa, alijiunga hivi karibuni na chama hicho, baada ya kujitoa CCM.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa leo amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Lowassa amechukua fomu hio Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mamia ya wanachama wa Chadema na viongozi wa juu wa Chama hicho.
Lowassa akiwasili makao makuu ya Chadema hii leo ikiwa ni siku chache baada ya kujiunga na chama hicho.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo na Edward Lowassa.
Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chadema.
Naibu Katibu Mkuu, Salum Mwalimu akiteta jambo na Edward Lowassa.
Lowassa akisalimiana na wanachama wa Chadema.
Wana Chadema wakimlaki Lowassa.
Lowassa na ujumbe wake wakiwa katika ofisi ya Mwenyekiti kuchukua fomu.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo baada ya kumkabidhi fomu Edward Lowassa kugombea Urais.
Edward Lowassa akizungumza jambo.
Lowassa na Tundu Lissu wakifurahia jambo 
Lowassa akiondoka baada ya kuchukua fomu.

No comments:

Post a Comment