.

.

.

.

Monday, November 09, 2015

UZINDUZI WA FILAMU MPYA YA JAMES BOND JIJINI DAR ES SALAAM



Mwigizaji Wema Sepetu  (kushoto) akifurahia jambo na mwakilishi wa  kampuni ya QWAY International inayosambaza kinywaji  cha Belvedere Vodka nchini, Tanya  Mulamula, wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market.



WATU mbalimbali walihudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya  James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market chini ya udhamini wa Belvedere Vodka, Heineken, Jaguar pamoja na Land Rover.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, mwakilishi wa kampuni ya QWAY International inayosambaza  kinywaji cha Belvedere Vodka,Tanya Mulamula alisema hafla hiyo inalenga kuwakutanisha wadau na kuifurahia filamu hiyo, ikiwa siku moja kabla ya uzinduzi wake.

Filamu ya hiyo ya Spectre iliyoigizwa na Daniel Craig kama James Bond ilizinduliwa rasmi hapa nchini Ijumaa iliyopita uzinduzi uliofana.

 
Alisema kuwa kinywaji hicho kinatambua nafasi ya filamu katika kuwaburudisha wateja wake na ndio maana imetoa tiketi nyingi za bure kwa wateja wake wengi.
 
" Belvedere Vodka, Heineken, Land Rover na Jaguar tumeamua kwa pamoja kuungana na watu wengine wengi katika kusherehekea uzinduzi wa filamu hii kwa kuanza na hafla hii ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa filamu yenyewe" alisema Tanya.
 
Pia Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya CMC inayohusika na magari ya Jaguar pamoja na Land Rover, Kim Withnall alisema kuwa filamu hiyo imehusisha magari ya Jaguar na Land Rovers na ndio maana hata kwa Tanzania kampuni yake imeshiriki katika kuandaa hafla hiyo


Wadau wa Belvedere Vodka pamoja na Heineken wakishow some love
Mchekeshaji ambae pia ni mshereheshaji Evance Bukuku akizungumza na Tanya Mulamula ambae ni mwakilishi wa  kampuni ya QWAY chini inayosambaza kinywaji cha  Belvedere Vodca pamoja na Moët-Hennessy  wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market
Mwakilishi wa  kampuni ya QWAY International inayosambaza kinywaji  cha Belvedere Vodka nchini, Tanya  Mulamula, kulia akiwa na Carlo wa Nyama Choma Festival wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market.
Bond Girls posing at the Belvedere Bar
Bond Girls posing at the Heineken DJ Booth


No comments:

Post a Comment