.

.

.

.

Saturday, December 12, 2015

BUNGE LA 11 NA VIMWANA WAHESHIMIWA ( VISU )


site_197_Swahili_329474


Wabunge warembo a.k.a visu ambao umri wao bado ni ‘asubuhi’, 
wabunge warembo wa kike ni wengi, lakini wafuatao ndiyo ‘shida’ kuanzia maumbo na sura zao.

magigeCATHERINE MAGIGE (CCM)
Rekodi ya urembo wake haijawahi kuvunjwa bungeni. Mara zote, tangu alipotinga bungeni mwaka 2010, amekuwa gumzo kubwa kwa uzuri wake, licha ya kushindanishwa na wabunge kadhaa, lakini bado ‘anatusua’ vilivyo.
BonnahBONNAH KALUWA (CCM)
Hii ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni. Uzuri na urembo wake umeonekana gumzo bungeni tangu mwanzo hadi mwisho wa kikao hicho. Sura, umbo na macho yake vimekuwa kivutio kikubwa.
kairukiANGELLA KAIRUKI (CCM)
Ukimwangalia vibaya, unaweza kusema ni shombeshombe. Urembo wa sura yake, umekuwa ukiwapa nyakati ngumu watu wengi, wakati mwingine kushindwa hata kung’amua kama ana asili ya Kiarabu au la! Kinachomuongezea sifa katika kilinge cha urembo ni umbo lake lililojengeka.
ESTER MATIKOESTER MATIKO (CHADEMA)
Achana na ukali wa hoja zake anapochangia mijadala. Hiki ni ‘kisu’ kikali kinachovutia bungeni. Umbo lake la ‘kitoto’, uzuri wa sura na macho ya mviringo, vinamfanya aonekane mrembo na mwenye uzuri wa kupindukia.
bukwimbaLOLESIA BUKWIMBA (CCM)
Tabasamu lake ndiyo limekuwa gumzo. Sura yenye uchangamfu imekuwa ikiteka macho ya watu wengi. Kamwe huwezi kuchoka kumtazama mwakilishi huyo. Mpole kama alivyo, lakini amekuwa ‘akikimbiza’ vilivyo mjengoni.

DK MARRY MWANJELWA (CCM)
Licha ya umri kuanza kumpigia honi lakini anawafunika wabunge wengi wenye umri mdogo. Urefu na figa nzuri, vinachangia kwa kiasi kikubwa kumweka kwenye orodha ya wabunge wa kike wanaotikisa kwa uzuri.

UMMY MWALIMU (CCM)
Hana makuu. Mpole na mwenye aibu wakati wote, lakini urembo wake unashereheshwa na umbo lake matata. Ana urembo wa haja unaoyapa macho kazi ya ziada kuitafuta kasoro yake.

CECILIA PARESSO (CHADEMA)
Urembo, uzuri wa umbo lake, urefu, unene wa wastani na sura nzuri vinatosha kumuingiza kwenye orodha hii.


shonza
JULIANA SHONZA (CCM)
Umbo lake ni la kawaida, lakini shughuli iko usoni. Achana na sehemu zingine za mwili, ukimtazama usoni tu utagundua ni kisu.


lucyLUCY MAYENGA (CCM)
Ni mrembo wa umbo na sura. Hahitaji maneno mengi kumwelezea, lakini ukweli unabaki palepale kuwa ni miongoni mwa wabunge warembo walioupa shida Mji wa Dodoma.


Mboni-MhitaMBONI MHITA (CCM)
Akiwa umbali kidogo kutoka mahali ulipo, unaweza kumchukulia kawaida! Shughuli ipo akikusogelea. Umbo na uzuri wake ni habari nyingine.

NEEMA MGAYA (CCM)
Rangi yake ya asili, ngozi laini, umbo namba nane na ucheshi wake, vinamtetea kuingia kwenye ulingo wa wabunge hawa warembo zaidi.

VICKY KAMATA (CCM)
Silaha kubwa aliyonayo ni midomo na macho! Geuza gazeti nyuma, mtazame tena Vicky, unaona? Si umbo, si sura, si macho, si mdomo, Vicky Kamata ni mrembo. Inatosha kusema hivyo tu.

JESCA KISHOA (CHADEMA)
Ni mrembo anayevutia kwenye viunga vya bungeni na inawezekana ndiyo maana aliyekuwa Mbunge wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila aliamua kuchukua jumla na kumweka ndani.
bulaya
ESTER BULAYA (CHADEMA)
Kama unahitaji kumpongeza muumba kwa kazi njema, wewe mtazame Ester Bulaya, si mrefu, si mfupi, si mweusi wala si mweupe. Yuko kati kwa kati. Akitembea, kama ni barabarani, jihadhari na vyombo vingine vya usafiri

No comments:

Post a Comment