.
.
Wednesday, September 24, 2008
WARIOBA AUNGURUMA
Tanzania kama Taifa lenye dola kamili (sovereign) litatikisika na kudhalilika mno machoni pa wananchi wake na katika jumuiya ya kimataifa, iwapo matajiri waliogushi na kuiba fedha za katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hawatafikishwa mahakamani. Onyo hilo limetolewa jana na waziri Mkuu wa zamani Jaji Joseph Sinde Warioba alipofanya mahojiano maalum jana, ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Jaji Warioba alisema kimsingi hatua za awali zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na mafisadi zina mwelekeo mzuri. ``Tutakuwa tumefanya makosa makubwa na ya kihistoria, kutowafikisha wezi kortini eti kwa sababu ni matajiri. Kosa hili litakuwa limeitikisa Tanzania kama nchi sovereign (Dola).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment