.

.

.

.

Saturday, October 25, 2008

FAMILIA YA JENNIFER HUDSON YAUWAWA

Kuna habari za kusikitisha. Mama yake mzazi Jennifer Hudson, Darnell Donerson (57), na kaka yake Jason Hudson (29), wameuwawa jana nyumbani kwao huko Chicago. Mpwa wake mwenye miaka 7 anatafutwa na polisi wametoa Amber Alert (tangazo maalum kwa ajili ya watoto waliohatarini). Polisi wanamshikilia William Balfour (27) ambaye ni mume kwa mdogo wake.Jennifer Hudson alipata tuzo la Oscar mwaka jana kwa ajili ya sinema, Dreamgirls. Aliigiza kama Effie White ambaye alikuwa mwimbaji mkuu wa kikundi cha Dreamgirls kabla ya kupinduliwa na Deena Jones (Beyonce). Jennifer alipata umaarufu kwenye American Idol

No comments:

Post a Comment