.
.
Monday, October 20, 2008
MTOTO ALBINO AUWAWA JANA
Wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi -Albino limeingia mkoani Shinyanga kufuatia mauji ya mtoto mmoja Albino katika kijiji cha Shilela, Kata ya Segese wilayani humo. Mtoto huyo wa kike aitwaye Esther Charles, mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika shule ya msingi kijiji hapo ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana. Diwani wa Kata ya Segese Bwana Joseph Mayala amesema watu wasiojulikana wakiwa na mapanga usiku wa manane walivamia nyumba ya Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Mzolewa Mashili ambaye ni baba wa mtoto huyo kwa kuvunja mlago wa nyumba yake kwa kutumia jiwe kubwa. Amesema watu hao waliwaweka chini ya ulinzi wazazi wa mtoto huyo na kuanza kumchuna sehemu za usoni, kichwa hadi ngozi ya kisogoni na kumkata miguu yake kuanzia sehemu za nyonga na kuondoka nayo. Diwani huyo amewataka wananchi wakiwemo walinzi wa jadi Sungusungu Wilayani Kahama kuhakikisha watu wanaojihusisha na mauaji hayo wanafichuliwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment