Katika kuhakikisha kuwa anajiandaa kibingwa kukabiliana na majabali ya muziki Hiphop kutoka USA...Lil Wayne..pamoja na The Game.... katika Tuzo za MTV Afrika (MTV Africa Music Awards) nafasi ya Mwanahip Hop Bora ....mchizi Joseph Haule a.k.a Profesa Jay...anajiandaa kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo kwa ajili ya kampeni za kuomba kura kwa masela wa hukoi .
Hayo yalithibitishwa hivi karibuni na mwakilishi wa MTV Bongo, Christine Mosha ,ambapo aliweka wazi kuwa kila anayeshiriki kwenye tuzo hizo ataenda katika nchi aliyopangiwa kwa ajili ya kuomba kura kwa mashabiki wa nchi husika.“Zimechaguliwa nchi nne kwa ajili ya washiriki kwenda kufanya kampeni, kwa upande wa Jay amepangiwa Kongo. Tutakuwa naye bega kwa bega kwa ajili ya kumpa tafu mtu wetu,” alisema.Aidha aliongeza kwamba, wanaamini kampeni ya Prof. Jay itaenda vizuri kutokana na kukubalika kwake katika nchi nyingi za Afrika hivyo atakwenda sambamba na wapinzani wake Lil Wayne na The Game wa Marekani.
No comments:
Post a Comment