.

.

.

.

Wednesday, October 01, 2008

STEVE NA WEMA


Habari zisizo na chembe ya shaka ambazo zimepatikana zinasema kuwa penzi la Kanumba na Wema limerudi ‘fresh’ na kwamba wawili hao wapo ‘kiupya zaidi’.Mmoja wa waleta habari muhimu amesema kwamba wawili hao hivi sasa wapo kama kumbikumbi, bibi mbele bwana nyuma kila wanapofanya ‘mitoko’ mbalimbali.“Wamerudiana, wanapendeza sana. Kanumba anamtembelea Wema mara kwa mara, Wema naye ni hivyo kwa kweli ‘couple’ yao inavutia,” alisema mleta habari kwa sharti la kuhifadhiwa jina.Mleta habari wetu mwingine alisema kuwa haishangazi mastaa hao kurudiana kwani ni kawaida ya wapenzi kuachana na kusameheana ila viapo walivyokula walipotengana mwaka jana ndivyo vinavyoleta mashaka.“Kanumba aliwahi kujiapiza kuwa hataongea milele na Wema lakini leo yako wapi? Hii inashangaza ila nawatakia uhusiano mwema,” alisema mtoa habari huyo.Alipoendewa hewani Kanumba ili aliongelee penzi lake na Wema lililofufuka, ‘kama kawa’ alikanusha na kudai kuwa ukaribu wake na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 unasababishwa na filamu mpya wanayocheza inayokwenda kwa jina Ba Intension.“Jamani wameanza tena, yule dada wa watu nipo naye kikazi lakini hata nikiwa naye kuna ubaya gani?” Alihoji ‘bwa mdogo’ Kanumba ambaye hivi sasa yupo UK kwenye ‘dili’ zake.Wema alipotafutwa hewani, simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda mrefu bila kupokelewa.Hata hivyo, licha ya Kanumba kusema yupo na Wema kwa sababu za kikazi, uchunguzi umebaini kuwa ni kweli wawili hao wamerudiana, hivyo majibu ya kwamba wapo ‘kifilamu zaidi’ siyo ya kweli.
KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS TZ

No comments:

Post a Comment