.

.

.

.

Friday, October 24, 2008

WASEMA HATA RAISI JK ANAWAJUA



KIKUNDI kilichojitenga na kanisa la Waadiventista wa Sabato kinachojiita Masalia kimesema kuwa bado kipo na "hata Rais Jakaya Kikwete anajua tunachokifanya," licha ya kuonekana kama wajinga kwa kile wanachokiamini.
Waumini hao wameweka kambi kwenye bonde la Tabata wakisubiri "sauti ya Mungu" kuwaamuru waende barani Ulaya kuhubiri injili bila ya kuwa na hati za kusafiria wala viza.
Wakizungumza jana, waumini hao walisema wao sio vichaa bali ni watu wenye akili zao timamu na wanajua wanachokifanya na kwamba utawala wa nchi hii unajua wanachokifanya.
"Hata Rais Jakaya Kikwete, bunge na mkuu wa mkoa huu anajua tunachokifanya na kwanini tupo hapa sasa," alisema mmoja ya waumini hao.
Walibainisha kuwa watu wanaowashangaa na kuwaona wajinga wao wanawaacha waendelee kufanya hivyo, lakini ipo siku wataelewa kuwa wao ni nani na walikuwa pale kwa sababu gani.
Awali waumini hao walisema kuwa hivi sasa hawana kitu cha kuzungumza bali hadi baada ya wiki moja.
Awali waumini hao walikuwa 17 lakini walikuwa wakiongezeka siku hadi siku na kufikia idadi ya watu 53 hadi sasa.

No comments:

Post a Comment