KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imechukua maamuzi mazito baada ya kupangua majina ya wagombea wa nafasi za uongozi wa ngazi ya taifa wa jumuiya zake, ukiwemo Umoja wa Vijana (UV-CCM) katika jitihada za kurejesha mshikamano.
Duru za habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam zinasema aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa UV-CCM, Nape Nnauye, ametupwa nje.
Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu, wagombea uenyekiti wa UV-CCM ambao waligawanya wanachama wa CCM, wameenguliwa na badala yake nafasi hiyo imekwenda kwa Wazanzibari, wakati katika Jumuiya ya Wazazi, wakili maarufu, Nimrod Mkono ameenguliwa.
Majina yaliyopendekezwa yatawasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu kilichopangwa kufanyika Dodoma Novemba 8 na 9 .
Alisema majina yaliyopitishwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa UV-CCM ni Hamad Masauni, Suleiman Hajji na Adila Vuai ambao wote wanatokea zanzibar.
No comments:
Post a Comment