.

.

.

.

Saturday, November 22, 2008

NKUNDA MJINI RUTSHURU


Kiongozi wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jenerali Laurent Nkunda amefanya mkutano katika mji mpya waliouteka wa Rutshuru, kwa kutaka kuonyesha nguvu na uasi unaofanywa na majeshi yake.
Mamia ya watu wa eneo hilo wamehudhuria mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira uliopo kilomita 70 kaskazini mwa mji wa Goma.
Jenerali Nkunda alikosoa mpango wa kusambazwa kwa majeshi ya ziada 3,000 ya Umoja wa Mataifa, akisema kuwa hawatoleta amani.
Mapigano eneo hilo yamesita kwa siku mbili sasa, huku kukiwa na makubaliano ya kusitisha mapigano eneo hilo.
Mwandishi aliyekuwepo kwenye mkutano huo, alisema Jenerali Nkunda alikaribishwa kwa nyimbo alipoingia kwenye uwanja huo, na akatumia nafasi hiyo kucheza na mtoto.
Lakini mwandishi wetu alisema waliohudhuria mkusanyiko huo hawakuonyesha kumwamini sana kiongozi huyo na kwamba kuwepo kwake eneo hilo kumeleta tu hofu.
Pia makofi waliyokuwa wakiyapiga watu hao yalikuwa ni yenye kusita.

No comments:

Post a Comment